
Sitti bin Saad
SITI Bint Saad ni mwimbaji mkongwe nchi aliyetokea kwenye familia dunia ambaye alibarikiwa kipaji cha pekee cha uimbaji.
Kipaji
cha muimbaji huyo kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake
kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa
akimsaidia kuvitembeza.
Siti
alijaliwa kuwa na sauti iliyoweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili
nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vyao
vinapita.
Nguli
huyo alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama simba kutokana na
alivyoweza kupaza sauti yake mbali bila kuachia pumzi.
Historia
inaonyesha kwamba Siti alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari
mwaka 1880 na baada ya kuzaliwa alipewa jina la 'Mtumwa' kwasababu
alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na
mkabaila mmoja wa kiarabu.
Baba
yake Mzee Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa
ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari.
Hali
ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha
zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza
na kuzimudu vizuri.
Kama
waswahili wasemavyo 'kuzaliwa masikini si kufa masikini' Siti kipaji
cha uimbaji alichobarikiwa muimbaji huyo kilimsaidia siku za awali za
maisha yake na alitumia kipaji hicho kuuza vyungu vya mama yake.
Kutokana
na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi
kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya kusoma Kurani.
Mnamo
mwaka 1911 alihamia mjini ili kubooresha maisha yake.Ujio wake wa
kuishi mjini ulikuwa wa neema kwani ulimkutanisha na muimbaji wa kundi
la muziki wa taarabu la "Nadi Ikhwani Safaa" Muhsin Ali.
Katika
kipindi hicho, kundi la Nadi Ikhwani Safaa lilikuwa kundi pekee la
muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa
Seyyid Barghash Said.
Kundi
hilo lilikuwa la wanaume peke yake , wanawake hawakuruhusiwa kujiunga
na vikundi vya muziki kwani ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni.
Hata
hivyo Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea
kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu.
Baada
ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenziwe wa Nadi Ikhwani
Safaa ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali
katika jamii.
Walipata
mialiko mingi iliyokuwa ikitoka kwa Sultani na matajiri wengine wa
kiarabu na walimtumia kwenye maonyesho mengine yakiwemo ya harusi.
Inasemekana
ulifika wakati ambapo sherehe zilishindwa kufana kama Siti hakuwepo
kutumbuiza kwani alikuwa moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa
haraka hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika.
Hali hiyo ilisababisha Siti afananishwe na muimbaji wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri Umm Kulthum.
Mwaka
1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice
yenye makazi yake Mumbai India ilisikia umaarufu wa muimbaji huyo na
ikamwalika pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili
ili kujaribu kama muziki wake utauzika.
Kampuni
hiyo haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa
kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzwa katika kipindi cha miaka
miwili ya mwanzo na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa.
Kutokana
na kusambaa kwa santuri hizo umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu
kutoka sehemu mbalimbali za dunia walifika Zanzibari kuja kumwona
muimbaji huyo.
Mambo
yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi
ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki Zanzibar mahususi
kwa muimbaji huyo.
0 comments :
Post a Comment