Tabia za taarab
Taarab ni muziki ya Waafrika wa pwani iliyopokea athira kutoka
tamaduni nyingi hasa muziki ya Waarabu na Wahindi. Kimsingi ni uimbaji
wa mashairi unaofuata muziki wa bendi. Bendi hizi hutofautiana kieneo;
katika taarab wa Unguja vinanda vya kulingana na tarab za Kiarabu hupendelewa; katika taarabu wa Mombasa aina za ngoma ni muhimu; katika taarab wa Tanga gitaa inapendwa. Siku hizi vyombo vya kisasa vimetumiwa pia.
Historia
Neno "taarab" laaminiwa lina asili katika Unguja ambako mnamo 1870 Sultani Sayyid Bargash alialika kundi la wanamuziki kutoka Misri kuja Zanzibar
walioleta uimbaji wao aina ya "tarab". Alipopenda muziki hii sultani
alimtuma Mzanzibari Mohammed bin Ibrahim kwenda Misri ajifunzi vyiombo
vya huku. Mohammed aliporudi alikuwa mwanashairi wa Sultani akaendelea
kuwafundisha marafiki vinanda vyake. Pamoja waliunda kundi la Nadi Ikhwani Safaa inayosemekana ni bendi ya kwanza iliyotumia jina la "taarab".[1]. Kundi limeendelea hadi leo na kujulikana sasa kwa jina la "Malindi Taarab"[2].
Hata hivyo muziki ya Waswahili inayojulikana leo kwa jina la taarab
lina asili ya kale kushinda jina hili ambalo ni kawaida siku hizi. Kuna
kumbukumbu kutoka Lamu
ya muziki iliyoitwa "kinanda" iliyounganisha uimbaji pamoja na chombo
cha kibangala na ngoma ndogo na waimbaji wake walihamia Zanzibar
wakaitwa "taarabu" huko.
Taarab katika utamaduni wa Uswahilini
Katika utamaduni wa Waswahili taarab ilikuwa utamaaduni wa pekee kwa
sababu ilikuwa mahali pa pekee ambapo wanawake walifika kwenye jukwaa
pamoja na wanaume na kuimba. Kwa sababu hii taarab imepingwa mara kwa
mara na viongozi wa kidini walioona aina kadhaa za taarab ni haramu hazilingana na masharti ya dini hasa wakati wa mwezi wa Ramadhani na kama watu wanaanza .[3]kucheza
Miaka ya nyuma muziki ya taarab imesambaa hata barani nje ya
utamaduni wa Waswahili inavuta wasikilizaji katika miji mikubwa kote
Afrika ya Mashariki hadi Burundi na Rwanda. Bendi mbalimbali zimeingiza vyombo vya kisasa vya muziki katika mtindo wao kama vile keyboard na gitaa ya umeme.
Viungo vya Nje
- Mifano ya muziki ya taarabu (audio)
- Mwambao.com juu ya "tarabu"
- Ntarangwi, Mwenda: A Socio-Historical and Contextual Analysis of Popular Musical Performance among the Swahili of Mombasa, Kenya; in: Cultural Analysis 2001, 2: 1-37, 2001 University of California
- Igobwa, Everett Shigenje: Taarab and Chakacha in East Africa, 2007
- Vikundi vya muziki vya Zanzibar
0 comments :
Post a Comment