
ONYESHO MAALUMU LA USIKU WA MFALME MZE YUSSUF LITAFANYIKA NDANI YA DAR LIVE- MBAGARA
ONYESHO HILO AMBALO LIMEPEWA KAULI MBIU YA "MWACHE MFALME AITWE MFALME"
LITASHUHUDIA MZEE YUSSUF AKIWA NA BAND YAKE YA JAHAZI MODERN TAARAB AKIIMBA NYIMBO ZAKE ZOTE KALI AMBAZO AMEIMBA KUANZIA MIAKA YA 90 MPAKA KUFIKIA KILELE CHA MIAKA 11 YA MUZIKI WAKE HUU WA TAARAB 2015.
IKUMBUKWE TU KWAMBA TANGU ANZE KUIMBA NI MIAKA MINGI SANA ILA KWENYE MUZIKI HUU WA TAARAB NI MIAKA 11 SASA TANGU KUINGIA KWAKE STUDIO KU RECORD NYIMBO YA KWANZA MPAKA SASA
Onyesho maalum la Usiku
wa Mfalme Mzee Yussuf litafanyika ndani ya Dar Live Mbagala Jumamosi
April 25.
Onyesho hilo ambalo limepewa kauli mbiu ya “Mwacheni Mfalme aitwe
Mfalme” litashuhudia Mzee Yussuf kupitia kundi lake la Jahazi akiimba
nyimbo zake zote kali tangu aanze kuimba taarab.
Hiyo itajumuisha hadi nyimbo alizoimba akiwa na Zanzibar Stars Modern
Taarab.
Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo linafanyika kwa mara ya
pili katika historia yake. Mara ya kwanza lilifanyika zaidi ya miaka
mitano iliyopita katika ukumbi wa Travertine Hotel jijini Dar es Salaam.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/04/usiku-wa-mfalme-mzee-yussuf-dar-live.html
Copyright © saluti 5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/04/usiku-wa-mfalme-mzee-yussuf-dar-live.html
Copyright © saluti 5
0 comments :
Post a Comment