mzee yussuf apokelewa kama rais mkoani morogoro tazama hapa

si vijana wala wamama wakina baba wote walimpokea kwa shangwe mfalme mzee yussuf na kumsifu kwa nyimbo mbali mbali za makabila yanayo patikana mkoani morogoro na wengine wakampa mialiko ya kupata chakula cha jioni yote hayo kwa jili ya kazi yake nzuri.
Mfalme mzee yussuf juzi alifanya onyesho la kufa mtu ndani ya mkoa wa moro goro kisa cha kufanya watu wajione wako kwenye fukwe za bahari wakati hakuna bahari moro goro zaid fatilia picha za matukio hapa chini
 Prince amigo abubakar sudi lake jina akiwapa raha zaidi wakazi wa mji kasoro bahari morogoro akika ilikuwa siku ambayo kila mtu wa pale morogoro ambae alitembelea tamasha hilo la nguvu alitamani siku iyo isiishe kwa utamu na burudani ambazo zilikuwa zikiendelea pale makuti ndani ya jiji kasoro bahari
 Bibie kitoronto nae hakuwa nyuma kuhakikisha jaala haikimbiliki kwa wakazi wa morogoro
     ukimwita fatma ni sawa na ukimwita mcharuko pia ni sawa zaidi kutoka na kile ambacho anakifanya steji na kuwafanya watu waone viti vyao kama vina maji muda wote kutokana burudani ambayo bint huyu wa kizanzibar anainyoshe na umahiri wa kuimba na kucheza ndo unawafanya watu wapagawe kabisa na kuhisi vichwa vinapamba moto.
 Khadija yussuf sauti ya chiruku nae alihakikisha kuwa wapenzi wa jahazi wanapata kile ambacho walikiadi miezi ya nyuma kuwa jahazi litakapo tua nanga kwenye jiji lisilo kuwa na bahari patakuwa hapatoshi.khadija yussuf aliwapa raha na luwafanya wajihisi wapo nyumbani zaidi wanavyo fikilia
 Mussa mipango baba walda nae alihakikisha anasimama vyema kwenye safu ya wapiga muziki na kutoa muziki mzuri wa kuwapendeza watu hakika wakazi wa morogoro walisema kuwa show hii haijwai kutokea mjini hapo
 wakati huu wakazi wa morogoro walikuwa wakiusubiri kuliko wakati wowote wowote ule pale mfalme mzee yussuf aliposhika kipaza sauti na kuanza kusema nao kwa namna moja au nyingine nyuso za furaha zilionekana dhahiri mfalme alipopanda tu watu walipagawa na wengine kuzima kwa kutoamini kile kilichotokea yaani burudani ya aina yake naweza sema ivyo.
                                  wakazi wa morogoro wakiwa wanacheza muziki wa jahazi modern taarab
 ayaa sasa mfalme akaanza kwa kusema 
mfalme:goma la jahazi cheza ohhh
mashabiki:cheza cheza cheza eee
mfalme:we cheza cheza ohh
mashabiki:cheza cheza eee 
aahhhh nacheka kwa furaha kwani kama ukupata burudani hii utakuwa umekosa uhondo
 mfalme mzee yussuf akiendelea kuchonga na wakazi wa morogoro
 mhhh mzuka ukapanda safu nzima ya jahazi modern taarab ambayo inaongozwa na khadija yussuf kulia,fatma mcharuko,mish mohamedi,kitoronto na mc mabobish mwansiti
 kama unavyo jua kipendacho roho ula nyama mbichi shabiki akishindwa kujizuia akamua aje kucheza kidogo na mfalme wa taarab mzee yussuf
 naweza se,a kuwa ilikuwa nzuri sana hapa tunamuona bibie mish mohamedi mtoto wa kizaramo akicheza sindimba la kizigua kidogo hapa na mfalme mzee yussuf
 fatma mama shughuli nae hakuwa nyuma nyuma kuhakikisha anacheza sindimba kisawa sawa
mfalme mzee yussuf akamaliza kwa ujana kidogo kukumbushia enzi kwa kucheza kiduku aaa ndio kiduku.
mzee yussuf alipoulizwa na mwandishi wetu wa jahazi modern taarab media crew kuhusu show hii alisema neno moja tu kuwa mfalme ni mfalme tuu awezi kuwa malkia ata siku moja

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment