{ Kenya Mombasa}
STREET KENYA (MOMBASA) Mkurugenzi wa jahazi modern taarab Seif Mgwaru ndani ya mombasa Kenya
Gari ya Band ya Jahazi modern taarab ikiwa kizalendo zaidi baada ya chidi boy kuiandika jina la tanzania nyuma ya gari uku gari hiyo ikiwa anaranda randa mitaa ya mombasa
Jahazi modern taraab ndani ya mombasa time hii kama unavyoona usafiri ndo huu una randa randa mitaaya kivuko cha mombasa watu wetu wa nguvu tulikutana nao pale palmcity
{ Kenya Mombasa}
{ Kenya Mombasa}
Burudani ilikuwa namna hii pale sauti ya chirikuu Mwansiti Mbwana alipo shika kipaza sauti na kuwapa {jaala haikimbiliki} wakazi wa kenya mombasa mwansiti mbwana pia ni kati ya wasanii sita ambao watakwenda itambulisha albam yetu mpya kabisa ya {chozi la mama}
Huyu ni Fatma Mcharuko au waweza muita Fatma Nyoro mtoto wa kizanzibar akiwapa {marupe rupe}wakazi wa mombasa nchini kenya kiukweli msanii huyu awapo stejini huwa akosei kabisa kwani ni hodari wa kuimba na kucheza tena ana staili ya peke yake na mungu kamjalia sauti yenye nakshi nakshi za kumtoa nyoka pangoni . Fatma Mcharuko pia ni kati ya wasanii sita ambao wata kwenda itambulisha albam yetu mpya ya chozi la mama uku yeye akiwa na nyimbo inayosema {ASOKASORO NI MUNGU}
Fans wetu wakiburudika kitanzania zaidi hali ya kuwa wapo kikenya zaidi
Prince Amigo Mzee wa kisengeli akiwapa sengeli watoto wa Mombasa yani raha kama nini kwa upande wetu tunamwita mapafu ya swala maaana anakimbiza sana awapo stejini mzee wa {full shangwe}huyu pia ni kati ya wale wasanii sita ambao watakwenda isindikiza albam yetu mpya ya chozi la mama yeye akiwa na nyimbo ya {tiba ya mapenzi} sasa sijui hii tiba itawatibia wangapi soon itakuji tiba hii usikose cd ya nakala halisi
Mama ya Mji mwite Malkia leyla Rashidi zaidi yao Ndani ya Mombasa Usiku huu akiwa shusha na kuwapandisha na kuwatia kwenye dustbeen. Yani mombasa rahaaa siku hii mwanamke huyu ilifanya iwe ya nakshi nakshi kwa kucheza kwa maringo na madaha akiwa stejini.
Malkia Leyla rshidi pia ni kati ya wasanii sita ambao watakwenda isindikiza albam yetu mpya ya {chozi la mama} uku yeye akiwa na kibao kinacho sema (Fanya yako)
Mzee yussuf {big dady} huyu sasa ndiye kinara wa hii albam. Hapa alikuwa anaimba chozi la mama na hapo nyuma waki itikia kwa sauti zenye hisia kali kwani mashairi ya nyimbo hii yame tungwa kwa umakini zaidi ili kuleta ujumbe kwa watu ambao wanazarau mama zao na kuto kujua nini maana ya mama.
STORY/PICTURE BY HAJI MABOVU
0 comments :
Post a Comment